Katiba
Lengo la Umoja wetu ni kuendeleza na kudumisha umoja wa kitaifa, ambao ndio msingi wa upendo na amani katika taifa letu.

 


Home Lengo la Umoja Mission History Benefits Officers Bylaws Katiba Celebrations Meetings Gallery Resources Events Community Business Financial Aid Contact-Comments


Katiba

KATIBA YA UMOJA WA KIZALENDO WA WATANZANIA

(TanzanianCommunity Organization)

I: MADHUMUNI

1.Kusaidiana katika matatizo yanayohusiana na  msiba na kuendeleza shughuli za kitamaduni

II: UANAUMOJA

  1. Mtu  yeyote anayekubaliana na madhumuni ya Umoja huu na anayejitegemea (na sio lazima anaishi California) anaweza kuwa mwanaumoja.
  1. Kutakuwa na kiingilio cha dola ishirini na tano ($25.00). [Wale ambao walishakuwa Wanaumoja kabla ya tarehe kumi na sita, mwezi wa pili (Februari), mwaka wa elfu moja mia tisa tisini na sita (2/16/1996) hawatahitajika kulipa kiingilio hicho].
  1. Mwanaumoja anatoa mchango dola kumi ($10.00) kila mwezi, Mwanaumoja akitaka anaweza kutoa mchango mpaka mwaka moja (miezi kumi na miwili) kwa wakati mmoja na sio zaidi.
  1.  Mwanaumoja anategemewa kuhudhuria mikutano ya Umoja.
  1. Mwanaumoja ambaye hatatoa mchango wake kwa muda wa miezi mitatu mfululizo atakuwa na siku tano za ziada kulipa. Mwanaumoja huyo atakubushwa kwa simu au barua au mjumbe wa Kamati ya Utendaji kabla ya siku hizo tano kufika. Kama hatakuwa amelipa katika muda huo ataeleweka kuwa amejitoa kuwa amejitoa  na hatatambuliwa na umoja.
  1. Mwanaumoja ataruhusiwa kujinga tena (bila kutoa kiingilio upya), ikiwa atatoa malimbilikizo ya michango yote kwa wakati mmoja, na pia atalipa miezi mitatu ya mbele.
  1. Ikiwa mwanaumoja atataka kurejea katika umoja baada na mwaka moja ( miezi kumi na miwili) au zaidi, itambidi alipe malimbikizo yote pamoja na kutoa kiingilio upya.
  1. Ikiwa mwanaumoja atapoteza mapato ( kama kupoteza kazi) na anajiona kuwa hawezi  kuendelea kotoa mchango, itabidi aitaarifu Kamati ya Utendaji. Uanaumoja wake utalindwa hata baada ya miezi mitatu. Hata hivyo baada ya hali yake kimapato kutengamaa, atawajibika kulipa malimbilikizo yake yote.

III. UTAWALA

Kamati ya Utendaji itakuwa na wanakamati wane (4) kamati ya utendaji ndiyo itakayoongoza shughuli za kila siku za umoja.

Wanaumoja watatu (3) watachaguliwa kila baada ya miezi mitatu, na kazi yao itakuwa ni kusaidiana na wajumbe wa kamati ya utendaji katika shughuli mbalimbali za Umoja.

1. A) Shughuli zote za umoja zitaongozwa na kutekelezwa na wajumbe saba (7)-yaani wajumbe wane (4) wa kamati wa Utendaji, na wajumbe watatu (3) watakaochaguliwa kila baada ya miezi mitatu (3).

B) Kila mjumbe wa kamati ya Utendaji atahudumia kwa muda wa miaka miwili.

2.  Mjumbe wa kamati ya utendaji akiachia kazi yake kwa kujitoa, kwa    ugonjwa, au kwa  kutolewa, nafai iliyowazi itajazwa na mjumbe atakayechaguliwa na wanaumoja wote. Lakini iwapo mjumbe huyo wa Kamati ya Utendaji ni mwenyekiti, katibu, au Mweka Hazina, hapo wajumbe wanaobaki, watajichagulia Mwenyekiti, Kaimu

Mwenyekiti, Mweka Hazina, au Katibu ipasavyo.

3.  Wajumbe wa kamati ya utendaji hawatalipwa au kupokea malipo ya aina yeyote kutokana na uongozi wao. Lakini wajumbe wa kamati ya utendaji wanaweza kurudishiwa fedha za binafsi walizotumia kw niaba au kwa ajili ya Umoja. Wajumbe wa kamati ya utendaji hawatakuwa na mkataba na Umoja, au kuwa na kazi y akulipwa na Umoja.

4.  Ni lazima theluthi mbili (2/3) za wajumbe wa kamati ya Utendaji au  wajumbe watano (5) wa kamati ya utendaji wawepo ili mkutano wa kamati hiyo utambulike kuwahalali.

5.  Wajumbe wa kamati ya utendaji wakipenda, au wakikubaliana, au wakiona ni vyema,  

Mwanaumoja yeyote wa umoja wa kizalendo anaweza kuwa mwenyekiti wa shughuli za Umoja wa Kizalendo za uzalishaji fedha (ukuzaji wa mfuko wa Umoja, n.k.).

6.  (A) Taratibu za Uchaguzi – Kabla ya Uchaguzi

(i)  Mkutano wa uchaguzi utakuwa na wanaumoja watu (3), ambao sio wajumbe wa Kamati ya Utendaji, kuongoza uchaguzi.

(ii) Katika mkutano huo wanaumoja watapendekeza majina ya wagombea  nafasi za kamati ya utendaji. Kila pendekezo ni lazima liungwe na wanaumoja watatu ili jina lifikiriwe.

(iii) Mkutano wa uchaguzi utahakikisha kuwa mgombea ambaye jina lake limependekezwa anakubali kuutumikia umoja kw amuda wa miaka miwili.

(iv) Matokeo ya uchaguzi yatatangazwa baada ya kupiga kura na yatathibitishwa.

(v)  Katiba itakuwa pia katika lugha ya kiingereza, hasa kwa manufaa ya wanaumoja wasio raia wa Tanzania. Lakini lugha itakayotumika katika mikutano ni Kiswahili.

(vi) Kila mjumbe au wajumbe wawili au zaidi wa Kamati ya Utendaji wanaruhusiwa kuitisha mkutano wa dharura wa wanumoja wote.

(B) Siku ya Uchaguzi

(i)                Kamati ya Uchaguzi itatangaza siku ya uchaguzi

(ii)             Kila mwanaumoja atakuwa na haki ya kupiga kura mara saba (7) kwa majina tu yaliyopendekezwa kwa nafasi saba.

(iii)           Matokeo ya uchaguzi yatatangazwa baada ya kura zote kuhesabiwa na kuthibitishwa na kamati ya uchaguzi. Wshindi saba ndio watakaokuwa wajumbe wa Kamati ya Uongozi na uchaguzi utakuwa umekamilika.

Return to top

7.
a. Mwenyekiti au wajumbe wawili au zaidi wa Kamati wa Utendaji wanaruhusiwa kuitisha mkutano wa dharura wa wanaumoja wote.

b. Wajumbe wa kamati ya Utendaji watakuwa na uwezo kuunda Mwongozo wa umoja kufuatana  na  mahitaji ya wanaumoja kwa wakati huo. Marekebisho hayo lazima yawe kwa maandishi na yawe na sahihi za wajumbe wote wa kamati ya ya utendaji wa wakati huo.

8.  Mjumbe wa kamati ya uongozi haruhusiwi kushughulika kikatiba na mwanaumoja kwa niaba ya umoja; anaweza tu akimbiwa na Kamati ya Utendaji. Mwenyikiti 

akisaidiwa na katibu-mweka hazina wanahitajiwa kutoa taarifa ya hali ya Umoja kifedha na kadhalika, mara moja kwa mwaka, hasa muda mfupi kabla ya mkutano wa wanaumoja wote.

9.  Mwenyekiti, akisaidiwa na Mweka Hazina atatoa taarifa ya fedha za Umoja mara moja kwa mwaka kabla ya mkutano wa wanaumoja wote.

10. Mjumbe au wajumbe wa kamati ya utendaji anaweza/wanaweza kutolewa kwenye kamati kwa sababu au bila ya sababu kwa jumla ya kura theluthi mbili (2/3) ya wanaumoja wote au kwa sahihi (petition) kiasi cha theluthi mbili ya wanaumoja wote au kwa kura tano (5) za wajumbe wa Kamati ya Utendaji.

11. Mweka Hazina, au mwanaumoja anayekuwa kama kiongozi anayeshughulika na zaidi ya dola elfu moja ($1,000) atatakiwa kuwa na kinga ya kifedha (bond security)kutoka kwenye kampuni inayoshughulikia masuala hayo. Gharama zote za “bond” hiyo zitalipiwa na Umoja.

12. Mjumbe yoyote wa Kamati ya Utendaji atakuwa na haki ya kukagua vitabu, rekodi, barua ya aina yeyote, na vitu vyote vya umoja wakati wowote bila kukatazwa.

IV: VIONGOZI

Mwenyekiti

  1. Mkuu wa Umoja wa Kizalendo atakuwa Mwenyeki, ambaye pia atakuwa mwenyekiti wa Kamati ya Utendaji. Kadhalika atakuwa mwenyekiti wa mikutano ya wanaumoja wote.
  1. Mwenyekiti ataitisha mikutano yote ya Umoja na ya Kamati ya Utendaji ya Umoja.
  1. Mwenyekiti atatekeleza kazi zote kama ilivyoamuliwa na Kamati ya Utendaji wakati wakikutana kihalali.
  1. Atahakikisha kuwa uamuzi na matakuwa vinatekelezwa kama ilivyoamuliwa na Kamati ya Utendaji ya Umoja.

Kaimu Mwenyekiti

  1. Atachukuwa nafasi ya mwenyekiti iwapo mwenyekiti hatakuwepo au mgonjwa.
  1. Kaimu mwenyekiti atatekeleza kazi kama itakavyoamuliwa na Kamati ya Utendaji ya Umoja.
  1. Iwapo mwenyekiti na kaimu mwenyekiti watashindwa kutokea kwa ajili ya ugonjwa au vinginevyo, basi wajumbe wa utendaji watamchagua mmoja kati yao kushikilia uenyekiti mpaka hapo mwenyekiti atakapokuwepo.

Katibu

Katika mikutano yote ya Umoja, katibu atachukua maoni yote na kuyatunza. Atatunza pia rekodi zote za umoja. Ataandika barua zote za Umoja na kuzituma ipasavyo. Atatunza orodha zote za wanaumoja, katiba ya umoja na maelezo yote mengine yahusinavyo na umoja. Kama mjumbe atashughulika na kazi za Umoja akisaidiana na wajumde wa Kamati ya Utendaji.

Iwapo katibu atakataa, au ashindwe kutekeleza kazi yake ilivyoelezwa hapo juu, kazi yake itachukuliwa na Mwenyekiti au Kaimu wake au mwanaumoja yeyote atakayechaguliwa na wajumbe wa Kamati ya Utendaji.

Mweka Hazina
 
  1. Kazi yake ni kupokea michango  na malipo ya kila mwanaumoja  na kutoa malipo kwa niaba ya Umoja. Pia atatoa taarifa ya fedha kwenye mikutano au mkutano wa mwaka wa wanaumoja wote. Yeye pamoja Mwenyekiti na Kaimu Mwenyekiti ndio pekee wanaoweza kutoa pesa kutoka benki.
  1. Mweka hazina atatunza kwa ukamilifu malipo yote ya umoja na kutunza stakabadhi na hundi zote za Umoja.
     
V: UKAGUZI WA FEDHA

1.     Kamati ya watu watatu (3) itachaguliwa na Kamati ya Utendaji  kutoka miongoni mwa wanaumoja, na itafanya kazi kama Kamati ya Ukaguzi wa fedha mpa ka kufikia mkutano wa mwisho wa mwaka wa  wanaumoja wote. Mkutano huo pia utachagua kamati mpya ya ukaguzi wa fedha yenye idadi ilele ya wajumbe (3). Ikiwa nafasi kwenye kamati hii itabaki wazi kwa sababu yoyote ile, itajazwa na mjumbe au wajumbe watakaochaguliwa kwenye mkutano wa kawaida au wa dharura wa wanaumoja wote. Wajumbe wa Kamati ya Utendaji ya Umoja hawaruhusiwi kuwa wajumbe kwenye kmati hii.  

2.  Baadaye kufuatana na maamuzi ya Umoja, Umoja unaweza kumwajili mtaalamu mwenye liseni ya utunzaji na ukaguzi wa vitabu vya fedha, ili aweze kuwa anafanya ukaguzi wa vitabu vya fedha za Umoja. Kabla ya kila mkutano wa mwisho wa mwaka, nakala ya taarifa ya ukaguzi wa fedha itatolewa. Mweka

Hazina atasoma taarifa hiyo kwenye mkutano wa wote wa mwisho wa mwaka.  

Return to top

VI: MISAADA

1.  Misaada itatolewa kwa ajili ya misiba tu. Ni matatizo ya msibva tu yatakayohalalisha msaada kutoka kwenye hazina ya umoja huu kupewa mwanaumoja aliyefiwa na:

a)     Mzazi (baba au mama)
b)     Ndugu wa kuzaliwa naye
c) Ndugu ambaye ni kama mzazi wa mwanaumoja (mzazi alikufa akiwa mdogo)
d) Mume, mke au mtoto wa mwanaumoja

2. 

a) Mwanaumoja akifiwa na mtu hapa marekani na anataka kupeleka maiti nyumbani atasaidiwa kwa kiasi cha asilimia arobaini (40%) ya fedha za Umoja, lakini kiasi hiki atachopewa kisizidi dola elfu mbili ($2,000.00) za Umoja.
b) Mwanaumoja akifiwa na mtu hapa marekanni na hataki kupeleka maiti nyumbani atasaidiwa kwa kiasi cha asilimia thelathini (30%) ya fedha za Umoja, lakini kiasi hiki atachopewa kisizidi dola elfu mbili ($2,000.00) za Umoja.
c) Mwanaumoja akifiwa na mtu nyumbani (nje ya marekani) na anataka kwenda nyumbani atasaidiwa kwa kiasi cha asilimia ishiri na tano (25%) yafedha za Umoja, lakini kiasi hiki atachopewa kisizidi dola elfu moja mia tano ($1,500.00) za Umoja.
d) Mwanaumoja akifiwa na mtu nyumbani (nje ya marekani) na hataki kwenda nyumbani atasaidiwa kwa kiasi cha asilimia kumi na tano (15%) ya fedha za Umoja, kiasi hiki atakachopewa kisizidi dola mia tano ($500.00) za Umoja.

VII: VITI VILIVYO WAZI

Ikiwa Mwenyekiti, Kaimu Mwenyekiti, Katibu, au Mweka Hazina  wataacha viti vyao kwa kung’atuka au kwa sababu yoyote ile, Kamati ya Utendaji itamchagua mwanaumoja yeyote, au mjumbe wa Kamati ya Utendaji atamchagua mwanaumoja au mjumbe mwingine wa Kamati ya Utendaji kushikilia nafasi hiyo iliyowazi kwa muda tu uliobaki, mpaka uchaguzi mwingine utakapofanyika.

VIII: UMOJA UKIFA

Umoja ukifa, fedha za Umoja zitagawanywa ifuatavyo:

A) Kwanza: Umoja utalipa madeni yake yote pamoja na gharama za kufa kwake.

B) Pili: Kila mwanaumoja atarudishiwa fedha kulingana na malipo aliyoyatoa pamoja na riba kama ipasavyo. Ikiwa fedha zimetumika kama ilivyoelezwa katika katiba hii, na fedha zilizobaki hazitoshi kulipa kila mwanaumoja kama ilivyoelezwa hapo juu hapo basi fedha hizo zitagawanywa kati ya mwanaumoja kufuatana na makadirio ya wakati mwanaumoja alipojiunga kwenye Umoja.

IX: NAKALA YA KATIBA KWA WANAUMOJA

Katiba ya Umoja huu itachapishwa na kila mwanaumoja atapata nakala yake. Nakala za nyongeza zinazohusiana na mabadiliko ya kikatiba zitatawanywa kwa wanaumoja pale zinapokuwa tayari baada ya mabadiliko hayo kufanywa.

X: NYONGEZA (MABADILIKO)

Katiba hii inaweza kubadilishwa au kuongezewa, na mabadiliko hayo yanaweza kukubaliwa na kupitishwa kwa kura ya ziadi ya asilimia hamsini (50%) ya wanaumoja wakati wa mkutano wa kawaida au wa dharura ulioitishwa kwa ajili ya suala hilo tu; au kwa nyaraka za zaidi ya asilimia hamsini (50%) ya wanaumoja zilizotiwa sahihi na wanaumoja hao. Utaratibu wa kuthibitisha ukweli wa asili ya nyaraka hizo utatayarishwa na Kamati ya Utendaji ya Umoja.

XI: MSAMIATI ULIOTUMIKA  

Ufafanuzi wa msamiati ni kufuatana na jinsi ulivyotumika katika Katiba hii.

 1. Umoja: Umoja wa Kizalendo wa Watanzania wanaoishi nchini Marekani.

Return to top

NYONGEZA: 1

Nyongeza hii ni badiliko linalohusu Sehemu II Kipengele 1 cha Katiba hii, nayo ni kama ifuatavyo:

Wanaouhusiwa kujiunga katika Umoja huu ni kama ifuatavyo:

Raia yeyote wa Tanzania au yeyote mwenye asili ya Tanzania, mke au mume wa Mtanzania, na watoto wa Watanzania. Uhalai wa badiliko hili ni kuanzia leo Desemba 21,1996. Inathibitishwa kwamba katika badiliko hili hakuna jambo lolote linalokiuka Katiba ya Umoja.

NYONGEZA: 2

Nyongeza hii ni badiliko linalohusu Sehemu VI Kipengele 1 cha Katiba hii, nayo ni kama ifuatavyo:

Umoja huu utafungua akaunti ya kielimu katika benki kwa ajili ya watoto walioko chini ya umri wa miaka kumi na minane wa mwanaumoja aliyefariki dunia. Umoja atatoa mchango wa mara moja utakaowekwa katika akaunti hiyo, na kiasi cha mchango huo hakitazidi dola mia tatu ($300.00). Uhalali wa badiliko hili ni kuanzia leo Juni 26,1999. Inathibishwa kwamba katika badiliko hili hakuna jambo lolote linalokiuka Katiba ya Umoja.

NYONGEZA: 3

Nyongeza hii ni badiliko linalohusu Sehemu II Kipengele 5 & 7 cha Katiba hii, nayo ni kama ifuatavyo:

Mwanaumoja atasimamishwa uanachama ikiwa atashindwa kulipa ada ya Umoja kwa muda wa miezi ishirini na minne (24) mfululizo. Mwanaumoja huyo anaweza kujiunga upya katika Umoja mara baada ya kipindi hicho ikiwa, lakini atatakiwa kulipa upya kiingilio cha dola hamsini ($50.00). Uhalali wa badiliko hili ni kuanzia leo Machi 24, 2001. Inathibishwa kwamba katika badiliko hili hakuna jambo lolote linalokiuka Katiba ya Umoja.

NYONGEZA: 4

Nyongeza hii ni badiliko linalohusu Sehemu II Kipengele 3 cha Katiba hii, nayo ni kama ifuatavyo:

Mwanaumoja atawajibika kulipa ada ya $15.00 kwa mwezi. Uhalali wa badiliko hili ni kuanzia leo Septemba 29, 2001. Inathibishwa kwamba katika badiliko hili hakuna jambo lolote linalokiuka Katiba ya Umoja.

NYONGEZA: 5

Nyongeza hii ni badiliko linalohusu Sehemu VI Kipengele 3 cha Katiba hii, nayo ni kama ifuatavyo:

Kutakuwepo kipindi cha miezi mitatu (3) ambacho mwanaumoja mpya atasubiri kabla ya kuwa na uhalali wa kupata msaada wa fedha za Umoja. Uhalali wa badiliko hili ni kuanzia leo Septemba 29, 2001. Inathibishwa kwamba katika badiliko hili hakuna jambo lolote linalokiuka Katiba ya Umoja.

NYONGEZA: 6

Nyongeza hii ni badiliko linalohusu Sehemu II Kipengele 5, 6 & 7 cha Katiba hii, nayo ni kama ifuatavyo:

Mwanaumoja atasimamishwa uanachama ikiwa atashindwa kulipa ada ya Umoja kwa muda wa miezi kumi na miwili (12) mfululizo. Mwanaumoja huyo anaweza kujiunga upya katika Umoja mara baada ya kipindi hicho ikiwa, lakini atatakiwa kulipa upya kiingilio cha dola hamsini ($50.00), na pia atalipa ada ya miezi mitatu ya mbele. Uhalali wa badiliko hili ni kuanzia leo Mei 3, 2003. Inathibishwa kwamba katika badiliko hili hakuna jambo lolote linalokiuka Katiba ya Umoja.

NYONGEZA: 7

Nyongeza hii ni badiliko linalohusu Sehemu VI Kipengele 2A cha Katiba hii, nayo ni kama ifuatavyo:

Ikiwa familia ya marehemu ina zaidi ya mwanaumoja mmoja katika Umoja huu na ikaamua kumsafirisha maiti nyumbani, Umoja utatoa asilimia arobaini (40%) ya pesa za zilizopo, lakini kiasi atakachopewa kisizidi dola elfu nne ($4,000.00) kwa vile ni kifo kimoja, bila kujali idadi ya wanaumoja katika familia hiyo. Ikiwa vitatokea vifo zaidi ya kimoja katika familia moja kwa wakati mmoja, Umoja utatoa asilimia arobaini (40%) ya pesa zilizopo kwa kila kifo. Hata hivyo, kitakachotolewa kwa kila kifo kisizidi dola elfu nne ($4,000.00). Uhalali wa badiliko hili ni kuanzia leo Mei 3, 2003. Inathibishwa kwamba katika badiliko hili hakuna jambo lolote linalokiuka Katiba ya Umoja.

NYONGEZA: 8

Nyongeza hii ni badiliko linalohusu Sehemu VI Kipengele 2B ya Katiba hii, nayo ni kama ifuatavyo:

Ikiwa mwanaumoja amefiwa na jamaa yake hapa Marekani na akaamua kumzika hapa, atasaidiwa kwa kiasi cha asilimia thelathini (30%) ya fedha za Umoja zilizopo, lakini kiasi hiki atachopewa kisizidi dola elfu mbili ($2,000.00). Ikiwa familia ya marehemu ina  zaidi ya mwanaumoja mmoja katika Umoja huu na familia ikaamua kumzika marehemu hapa Marekani, Umoja utaipa familia hiyo nyongeza ya dola elfu moja ($1,000.00). Kiasi hicho hata hivyo hakitazidi dola elfu tatu ($3,000.00). Uhalali wa badiliko hili ni kuanzia leo Mei 3, 2003. Inathibishwa kwamba katika badiliko hili hakuna jambo lolote linalokiuka Katiba ya Umoja.

NYONGEZA: 9     

Nyongeza hii ni badiliko linalohusu Sehemu VI ya Katiba hii, nayo ni kama ifuatavyo:

Umoja huu utaongeza Kipengele 2E cha Sehemu VI ya Katiba hii. Mwanaumoja akifa na familia yake ikaamua azikwe hapa Marekani, Umoja utatoa kiasi cha asilimia thelathini (30%) ya pesa za Umoja zilizopo. Kiasi hiki hata hivyo kisizidi elfu mbili ($2,000.00). Ikiwa familia ya marehemu mwanaumoja itaamua kusafirisha mwili wake nyumbani, umoja utatoa kiasi cha asilimia arobaini (40%) ya pesa za Umoja zilizopo. Kiasi hicho hata hivyo kisizidi dola elfu nne ($ 4,000.00). Uhalali wa badiliko hili ni kuanzia leo Mei 3, 2003. Inathibishwa kwamba katika badiliko hili hakuna jambo lolote linalokiuka Katiba ya Umoja.

NYONGEZA: 10

Nyongeza hii ni badiliko linalohusu Sehemu II Kipengele 4 cha Katiba hii, nayo ni kama ifuatavyo:

Ikiwa mwanaumoja atakosa kuhudhuria mikutano mitatu (miezi tisa) mfululizo bila sababu muhimu*, atawekwa katika kipindi cha uangalizi. Ikiwa mwanaumoja atakosa kuhudhuria mikutano minne mfululizo (miezi kumi na miwili) bila sababu mihimu, itatambulika kuwa mwanaumoja huyo amejitoa kwenye Umoja. Uhalali wa badiliko hili ni kuanzia leo Mei 3, 2003. Inathibishwa kwamba katika badiliko hili hakuna jambo lolote linalokiuka Katiba ya Umoja.

NYONGEZA: 11

Nyongeza hii ni badiliko linalohusu Sehemu III Kipengele 1A na 1B cha Katiba hii, nayo ni kama ifuatavyo:

Umoja wa Kizalendo utakuwa na Bodi ya Wakurugenzi. Bodi hii itakuwa na wajumbe tisa (9) ambao watachaguliwa kila baada ya miaka miwili. Kuundwa kwa Bodi hii kunaondoa mara moja nafasi ya wajumbe watatu waliokuwa sehemu ya kamati ya uongozi, ambao walikuwa wakichaguliwa kila baada ya miezi mitatu. Uhalali wa badiliko hili ni kuanzia leo Septemba 27, 2003. Inathibishwa kwamba katika badiliko hili hakuna jambo lolote linalokiuka Katiba ya Umoja.

bonyeza kupata Fomu ya Maombi katika

* Sababu ya kuwa kazini haiwezi kutolewa zaidi ya mara moja.

Return to top


website