Lengo la Umoja
Lengo la Umoja wetu ni kuendeleza na kudumisha umoja wa kitaifa, ambao ndio msingi wa upendo na amani katika taifa letu.

 


Home Lengo la Umoja Mission History Benefits Officers Bylaws Katiba Celebrations Meetings Gallery Resources Events Community Business Financial Aid Contact-Comments


Tamko La Lengo La Umoja
Lengo pana la umoja wetu (Tanzanian Community Organization) ni kuendeleza nakudumisha umoja wa kitaifa ambao ndio msingi wa upendo, amani na utulivu katika taifa letu, ambapo madhumuni ya Umoja kijumuiya ni kujenga jumuiya hai ya Watanzania kwa kuhamasisha wanajumuiya kujenga uhusiano wa kindugu miongoni mwao, na kuwasaidia kufikia malengo ya kinafsia na yale ya kijumuiya. Miongoni mwa malengo hayo ni kama vile kuelewa muundo wa kijamii wa taifa la Marekani, kufahamu na kufanya mabadiliko muhimu ya kitamaduni (mila na desturi) nchini Marekani, kujipatia elimu, na jinsi ya kujiandaa kwa ajira.  Sisi kama sehemu ya jamii ya Tanzania iliyoko mbali na nyumbani, pia tunataka kuchangia maendeleo ya kijamii, kielimu, na kiuchumi ya Tanzania kwa njia mbalimbali. Umoja wetu pia unapenda kujenga uhusiano mzuri na jamii nyingine za Kiafrika, vyama mbalimbali vya kijamii mahali tunapoishi, na jamii nzima kwa jumla kwa vile sisi pia ni sehemu ya jamii hiyo. Kwa kuhimiza umoja na ushirikiano miongoni mwa Watanzania hapa Marekani, Umoja wetu unaendeleza umoja wa kitaifa ambao hulifanya taifa letu kung’aa karibu na mbali.


website